TRA yajipanga kupambana na wakwepaji wa kodi

Na Dominic Allen

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Januari 09, 2026 imehitimisha kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa nusu mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika jijini Arusha kwa muda wa wiki moja, ambapo imekuja na mikakati mbalimbali ya kuzuia ukwepaji kodi na kuongeza wigo wa kodi.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda wakati akifunga kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), amesema kuwa TRA itaendelea kupambana na wakwepaji wa kodi kwa njia mbalimbali ikiwemo kuimarisha mipaka, kuzuia magendo na kuwa na mbinu mbalimbali.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda akizungumza wakati akifunga kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa nusu mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika jijini Arusha. (Picha na TRA)

Mwenda ameongeza kuwa lengo la TRA ni kuongeza wigo wa kodi kwa kusajili biashara mpya na kuwasajili wafanyabiashara ambao bado hawajaingia katika mifumo ya kulipa kodi.

“Haturidhiki na idadi ya walipakodi tulionao ikilinganishwa na idadi ya Watanzania hivyo kazi iliyopo mbele yetu ni kwenda kuongeza wigo wa kodi,” ameeleza Mwenda.

Baadhi ya maafisa pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika kwa muda wa wiki moja katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na TRA)

Aidha, amesema kuwa wataendeleza uadilifu kama ilivyo jadi ya TRA sambamba na utoaji wa elimu ya kodi, kuwasikiliza walipakodi, kuwezesha biashara zao na kutatua changamoto zinazowakabili walipakodi, huku akionesha shauku yake juu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuisaidia nchi kujitegemea.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW