Dkt. Slaa anyimwa dhamana kwa sababu ya usalama wake

Na Dominic Allen.

Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo imenyima dhamana Dkt. Wilbroad Slaa baada ya upande wa Jamhuri kuweka kiapo cha kupinga dhamana yake kwa sababu ya usalama wake na kutokamilika kwa upelelezi.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutoka Mahakamani, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amesema kitendo hicho cha kumnyima dhamana sio cha kiungwana kwani mawakili upande wa Dkt. Slaa walipaswa kufahamu juu kiapo hicho ili waweze kujibu hoja na kusisitiza kuwa dhamana ni haki ya kila mtuhumiwa.

Wakili Mwabukusi ameongeza kuwa yeye, Wakili Dickson Matata na Wakili Hekima Mwasipu wamepokea kiapo hicho na wapo tayari kuendelea na kesi hiyo.

Dkt. Slaa anakabiliwa na kesi ya kuchapisha za taarifa za uongo katika mtandao wa X kuhusu kuwepo kwa mawasiliano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ambapo mawasiliano hayo yanahusu kupeana fedha.

Hata hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha shauri hilo mpaka siku ya Jumatatu Januari 13, 2025.

Dkt. Wilbroad Slaa alikamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mbweni, Dar es Salaam ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mbweni na baadae kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Kati (Central Police) Dar es Salaam.

Picha: Mwananchi

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW