Watu 14 wamepoteza maisha na wengine 7 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kugongana na gari aina ya Coaster iliyokuwa ikitokea Morogoro usiku wa kuamkia leo Disemba 18, 2024 katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro, Nkungu Daniel amethibisha kupokea kwa miili ya waliopoteza maisha ambao ni wanaume 8 na wanawake 6 pamoja na majeruhi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro kutoa pole kwa majeruhi wa ajali hiyo wanaopatiwa matibabu, huku akitoa wito kwa wananchi kufika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kutambua miili ya wapendwa wao.
Katika ajali hiyo madereva wote wamepoteza maisha.


