Idadi ya watahiniwa wa kidato cha Nne yaongezeka hadi asilimia 13.2% kwa mwaka 2026

Idadi ya watahiniwa wa shule ambao wameanza kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (NECTA) mwaka 2026 imeongezeka kwa watahiniwa 74,202, sawa na asilimia 13.02, ambapo jumla ya watahiniwa 667,040 wameshaanza kufanya mtihani huo,  ikilinganishwa na watahiniwa 569,883 kwa mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohamed, jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa mtihani huo utamalizika Novemba 6, 2026, katika shule za Sekondari na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea nchini.

Kati ya watahiniwa hao, 644,085 ni watahiniwa wa shule, huku 22,955 wakiwa watahiniwa wa kujitegemea, ambapo watahiniwa wa shule, wavulana ni 297,309 na wasichana ni 346,776, huku kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, wavulana ni 10,223 na wasichana ni 12,732.

Jumla ya vituo 7,067 vitatumika kwa ajili ya kufanyia mtihani huo, zikiwemo shule za sekondari 6,265 na vituo 802 vya watahiniwa wa kujitegemea. Aidha, Profesa Mohamed ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha mtihani huo unafanyika kwa amani na utulivu.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW