Jamii ya Wahadzabe washauriwa kujenga nyumba imara za asili kukabiliana na El Niño

Ismaili Nyerere, Balozi wa Dwellers Check Hub kutoka jamii ya Wahadzabe, ametoa elimu kwa jamii hiyo kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na mvua za El Niño zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Jamii hiyo imeshauriwa kujenga nyumba imara za asili, ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, katika mafunzo haya yaliyofanyika kuanzia Septemba 24 hadi Oktoba 10, 2026, yakihusisha jumla ya wakazi 300 kutoka vijiji kadhaa, vikiwemo Kaqang’anged, Murus na Mbuga Nyekundu, vilivyopo Kata ya Baray, Tarafa ya Lake Eyasi, mkoani Arusha.

Ismail akitoa mafunzo kwa jamii ya Wahadzabe kuhusiana na namna ya kukabiliana na mvua za EI Nino kwa kuwashauri na kuwaasa wajenge nyumba imara ili kuimarisha usalama wao baada ya mvua hizo kutokea.

Kwa upande wao, jamii ya Wahadzabe, ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea uwindaji kwa ajili ya kujipatia chakula, imeiomba Serikali na wadau mbalimbali kuwapatia msaada wa maturubai na chakula, wakieleza kuwa mvua hizo zinaweza kuathiri shughuli zao za uwindaji na hivyo kuhatarisha upatikanaji wa chakula na mahitaji yao ya kila siku.

#InternationalMediaSupport #EuropeanUnion #UbaloziwaUswisiTanzania

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW