Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60 eneo la kusini mwa nchi hiyo wamepoteza maisha kufuatia kupasuka kwa Bwawa la Arba’at siku ya jumamosi, vyombo ya habari nchini Sudan vimeripoti.
Takribani watu 200 bado hawajulikani walipo kutokana na kupasuka kwa bwawa hilo huku taarifa kutoka Umoja wa Mataifa zikisema kuwa kabiria vijiji 20 vimeharibiwa na huku ikiziacha kaya 50,000 bila makazi.

Mvua zenye upepo mkali zimetajwa kuwa chanzo cha kupasuka kwa bwawa hilo ambalo ndiyo chanzo kikuu cha maji katika mji wa Bandari wa Sudan. Miundombinu katika maeneo yaliyokumbwa na janga hilo Sudan imeharibiwa vibaya.
“Eneo hili halitambuliki. Umeme na mabomba ya maji yameharibiwa” amesema Omar Eissa Haroun, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika Jimbo la Red Sea.
Nchi ya Sudan inakumbwa na janga hili ikiwa tayari ipo kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka sasa.
Mwandishi: Dominic Allen


