Baraza la Madiwani Ludewa lawafuta kazi kwa kusababisha hasara zaidi ya Tsh. Milioni 13

Na Amiri Kilagalila

Watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe waliokuwa kwenye Kamati ya Ukusanyaji wa Mapato, wamefutwa kazi mara baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa vilivyosababisha hasara kwa mwajiri ya zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 13.

Uamuzi huo umetolewa jana Juni 18, 2025 na Baraza la Madiwani Ludewa baada ya kikao maalum kilichojadili masuala ya nidhamu kwa watumishi wa umma, ambapo limefikia uamuzi wa kuwachukulia hatua kali watumishi hao ni Ezekia Mligo na Peter Alphonce kwa kujihusisha na vitendo vya ukiukaji wa maadili, wizi na rushwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Wise Mgina amesema hatua za kinidhamu pia zimechukuliwa kwa watumishi wengine wawili Anuciata Mapunda pamoja na Obothe Msemakweli, ikiwemo kukatwa 15% ya fedha kwenye mishahara yao kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kama sehemu ya kuwajibika kwa uzembe uliopelekea hasara kwa halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Wise Mgina akizungumza wakati wa kikao maalum kilichofanyika Juni 18, 2025 ambacho kilijadili masuala ya nidhamu kwa watumishi wa umma. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas amesema watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za utumishi wa umma, huku akisisitiza kuwa halmashauri hiyo haiwezi kufumbia macho ubadhilifu.

“Hakuna mtumishi wa Ludewa, kuna watumishi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Olivanus Thomas.

Baadhi ya Madiwani wa Ludewa mkoani Njombe ambao walishiriki katika kikao hicho. Picha na Amiri Kilagalila.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Ludewa Mjini, Bi. Monica Mchiro, waliwataka watumishi wote wa halmashauri hiyo kuwa waadilifu na kuzingatia maadili ya kazi zao, ili kujenga imani kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya wilaya.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW