TYC yawaita vijana kwenye kilimo, “Ni ajira yenye staha”

Na Amiri Kilagalila

Kufuatia changamoto ya ukosefu wa ajira Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Youth Coalition (TYC) limetoa wito kwa vijana kugeukia Sekta ya Kilimo kufuatia sekta hiyo kuwa na fursa nyingi za ajira kuanzia shambani, viwandani hadi masokoni.

Akizungumza hayo Mei 30, 2025 katika Ukumbi wa SHIPO Njombe Mjini mara baada ya majadiliano na vijana juu ya fursa na changamoto za kilimo biashara, Afisa Mradi wa YEFA Kilimo Sauti kutoka Shirika la TYC, Josephina Onesmo amesema kuwa kwa sasa vijana wanakumbana na changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Vijana ni kundi kubwa katika nchi yetu lakini pia ndio wanaopata changamoto sana ya ajira na wamekuwa na mitazamo kwamba kilimo ni shughuli ambayo inafanywa na vijana ambao hawajasoma hivyo tumekuja kuwafungua vijana waone kwamba kwenye kilimo kuna fursa na kunatengeneza ajira zenye staha” alisema Onesmo.

Nae Afisa Vijana mkoa wa Njombe ambaye pia ni Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Elia Kasanga amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo ya serikalini ili waweze kufanya kilimo chenye tija, huku Afisa Kilimo mkoa wa Njombe, Stella Kutona akisema Serikali ya Tanzania imeweka mikakati madhubuti ya kuwainua wakulima nchini.

“Tufuate kanuni tu mtafanikiwa kwa kuwa kwenye kilimo ndiyo kuna fedha, na sio kweli kwamba kilimo ni kwa ajili ya watu ambao hawajasoma” amesema Kutona.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria majadiliano hayo yalioangazia suala la vijana na fursa pamoja na changamoto za kilimo biashara. Picha na Amiri Kilagalila.

Kwa upande wake mkulima maarufu wa zao la Parachichi mkoani Njombe, Steven Mlimbila amewataka vijana wanaotaka kufanikiwa kwenye Sekta ya Kilimo kuwa na subira ya mafanikio pamoja na kuwa waaminifu kwenye biashara na mikopo.

Veronika Kihumbu ambaye ni miongoni mwa vijana walioshiriki katika majadiliano hayo ya kilimo akiwemo ameeleza matarajio yake.

“Kusoma kuna kupa upeo wa kufanya kitu kwa hiyo tuachane na kusubiri ajira za kukaa ofisini badala yake tujiajiri wenyewe katika suala la kilimo kwa kuwa ni biashara na ajira tosha, na tunaamini mafunzo haya yamekwenda kutuongezea kitu kwenye shughuli zetu” alisema Kihumbu.

Mwezi Mei 22, 2025 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Tsh. Trilioni 1.242 kwa ajili ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, ambapo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha katika Wizara ya Kilimo, Waziri Hussein Bashe alisema kuwa hadi sada katika eneo la ajira zilizotokanana utekelezaji wa miradi ya kilimo, Wizara hiyo imezalisha ajira za kudumu na za muda mfupi 1,084,481 kupitia programu na miradi mbalimbali ya maendeleo ya kilimo ikiwemo miradi ya uzalishaji na utafiti; ujenzi, ukarabati na usanifu wa miradi ya umwagiliaji, programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora na Vyama vya Ushirika.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW