Mwabukusi: Je lipi bora ‘Kujipanga kuingia kwenye uchaguzi’ na ‘Kujipanga na uchaguzi’?

Na Wakili Boniface Mwabukusi

KUNA KUJIPANGA KUINGIA KWENYE UCHAGUZI NA KUJIPANGA NA UCHAGUZI

Je lipi bora “Kujipanga kuingia kwenye uchaguzi” na “Kujipanga na uchaguzi.”?

1. Kujipanga kuingia kwenye uchaguzi, hili linamuhusu mtu au kikundi cha watu wanaotaka kushiriki kama wagombea au washindani katika uchaguzi. Mtu anayejipanga kuingia kwenye uchaguzi ana sababu kama:

(a) Nia ya kugombea nafasi fulani ya uongozi.

(b) Kutengeneza mtandao wa kisiasa na uungwaji mkono.

(c) Kujenga ajenda na sera zake kwa wapiga kura.

(d) Kutafuta wadhamini na rasilimali za kampeni.

(e) Kuhakikisha anakidhi masharti ya kisheria na kikanuni ili kutoenguliwa. Kimsingi mtu huyu au chama cha namna hii hakichukui uchaguzi kama njia ya wananchi kushiriki kupata viongozi bora bali kama njia ya mtu au muhusika kuhodhi madaraka fulani na yanakuwa ni matamanio binafsi, kundi fulani na mara nyingi maslahi ya Taifa hayawi kipaumbele chake zaidi na kwake yeye uchaguzi ni jukwaa la kufanikisha lengo lake la kupata nafasi ya uongozi.

2. Kujipanga na uchaguzi, hili ni lengo la watu timamu ambao mara zote hulitazama Taifa kizalendo. Hawa ni wale wanaouangalia uchaguzi kwa mtazamo mpana zaidi, si lazima wawe wagombea au vyama vya siasa, lakini wanaweza kuwa:

(a) Wanaharakati wa kidemokrasia na haki za binadamu.     

(b) Wapiga kura wanaotaka kushiriki kwa uelewa.

(c) Vyombo vya habari vinavyofuatilia mwenendo wa uchaguzi.

(d) Asasi za kiraia, Asasi za kitaaluma, Madhehebu ya dini na waangalizi wa uchaguzi.

(e) Vyama vya siasa vinavyotaka kulinda haki ya uchaguzi. Yaani vyama vinavyotambua kwamba ili uchaguzi uwe wa wazi, haki na halisi lazima sanduku la kura ndiyo litoe kiongozi na si vinginevyo.

(f) Kwa watu wanaoamini katika falsafa hii uchaguzi si tu kuhusu kushinda nafasi ya uongozi, bali pia kuhakikisha kuwa mchakato wote wa uchaguzi unakuwa huru, wa haki na wa uwazi.

(g) Ni watu wanaopenda kuwa na infirmed electorate na siyo mpiga kura anayehongwa kipande cha samaki, mshikaki au kibaba cha unga hawa huhamasisha uandikishaji wa wapiga kura, kufuatilia na kudai sheria na taratibu sahihi za uchaguzi kutoa elimu ya uraia kwa jamii kuhusu umuhimu wa uchaguzi ,kuuchunguza na kufichua udanganyifu au ukiukwaji wa haki za uchaguzi katika mazingira yote kuanzia uandikishaji, ugawaji wa Majimbo, usambazaji wa vifaa vya kupigia kura, uandaaji wa wasimamizi, wagombea na uteuaji wa mawakala wao.

Muhimu kutambua kwamba ni vyema zaidi kujipanga kwa uchaguzi kuliko kujipanga kuingia kwenye uchaguzi, kwani mtu anayejiandaa kuingia kwenye uchaguzi anaangalia ushindi wake binafsi au wa chama chake. Mtu anayejiandaa na uchaguzi anaangalia mustakabali wa demokrasia na haki za kila mpiga kura na anachagua zoezi la kupiga kura kama mchakato wa kuelekea kupata taasisi imara za kiutawala, yaani Mahakama, Bunge na Serikali ambavyo vyote vitawajibika katika hali ya check and balance huku wakishindana kuwajibika kwa Umma na siyo kwa mtu au kikundi cha watu wa chache.

Uchaguzi wenye afya unahitaji vyote viwili wagombea waaminifu na waangalizi wa haki, ndipo tunapata mfumo wa kisiasa uliyo huru na wa haki.

Mwandishi:
Wakili Boniface Mwabukusi
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW