Ishiba: Ushuru wa Marekani unaweza kuvuruga uchumi duniani

Na Dominic Allen

Waziri Mkuu wa Japani, Shigeru Ishiba leo Aprili 14, 2025 amesema kuwa ushuru ambao umewekwa na Marekani unaweza kuvuruga uchumi duniani, ambapo ametahadharisha kuhusu madhara ambayo tayari yametokana na maamuzi ya Rais Donald Trump kwenye uchumi wa dunia.

Waziri Ishiba amebainisha hayo wakati akizungumza katika Bunge la Japan, ambapo ameongeza kuwa Japani itatafuta mwafaka na Marekani kuhusu jinsi nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana katika masuala yanayohusu biashara na usalama wa kitaifa.

“Wakati wa mazungumzo na Marekani, tunahitaji kuelewa kilicho nyuma ya hoja za Trump, kwa kuzingatia mantiki na hisia zake” Ishiba aliliambia Bunge la Japan.

“Ninatambua kikamilifu kwamba kile kilichotokea hadi sasa kina uwezo wa kuvuruga utaratibu wa kiuchumi wa dunia” amesema Ishiba.

Waziri Ishiba amezungumza hayo kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya biashara na Marekani siku ya Alhamisi juma hili, ambayo yanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ushuru na vikwazo visivyo vya ushuru, viwango vya ubadilishaji wa fedha na mengineyo.

Ikumbukwe kuwa katika mvutano wa hivi karibuni kuhusu ushuru, Rais Trump alisema kwamba siku chache zijazo atatangaza kiwango cha ushuru kwa vipuri vya kielektroniki vinavyoagizwa kutoka nje ya Marekani.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW