Mfanyabiashara maarufu na mgombea Urais wa chama cha Republican, Donald Trump ameshinda Urais kwa kura (Electoral votes) 277.
Trump ambaye anakuwa Rais wa 47 wa taifa hilo anarejea tena katika Ikulu ya White House baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Kamala Harris. Kwa sasa Donald Trump anakuwa ni Rais mteule hadi pale atakapoapishwa.


