Dkt. Ntuli ashinda kwa kishindo Ukurugenzi Mkuu wa ECSA – HC

Na Kuni Atley (WAF)

Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dkt. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Dkt. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.

Dkt. Ntuli Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo, ataongoza kwa muda wa miaka mitano.

Dkt. Ntuli Kapologwe akipokea salamu za pongezi baada ya kushinda kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uchaguzi Februari 12, 2025, Waziri wa Afya nchini Tanzania, Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa nafasi hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba (7) walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.

Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa zoezi la uchaguzi.

Waziri Mhagama amesema mara baada ya usaili uliofanywa na Kamati ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa nchi wanachama, Dkt. Kapologwe alipata alama za juu zaidi na kuingia katika hatua ya mwisho pamoja na wagombea wengine wawili kutoka Kenya na Malawi.

Ameeleza kuwa majina ya wagombea hao watatu yaliwasilishwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA – HC), ambapo Dkt. Kapologwe ameibuka mshindi.

Kwa ushindi huu ni dhahiri ya kwamba Tanzania inaendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa ina Watalaam wenye sifa stahiki za kushika hatamu za Uongozi kwenye Jumuiya au Mashirika ya Kimataifa na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya wengi katika uboreshaji wa huduma za Afya.

“Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushika nafasi hii katika kipindi cha miaka 51 cha Jumuiya hiyo, kwani kwa mara ya kwanza, Mtanzania Dkt. Winny Mpanju alihudumu kama Mkurugenzi Mkuu kati ya mwaka 1983 na 2000. Ni mafanikio makubwa kuona Tanzania inapata nafasi hii tena baada ya miaka 27” amesema Waziri Mhagama.

Jumuiya ya ECSA – HC ilianzishwa mwaka 1974 na inajumuisha nchi tisa (9) ambazo ni Tanzania, Malawi, Kenya, Lesotho, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Uganda pamoja na Eswatini na inashirikiana na nchi 13 zisizo wanachama ambazo ni Botswana, Burundi, Cameroon, Eritrea, Gabon, Liberia, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Seychelles, Sudan ya Kusini, Sudan na Somalia.

Wajumbe wa Tanzania wameshangilia ushindi huo, huku wakimpongeza mgombea wake aliyependekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi hiyo.

Jumuiya ina jukumu la kukuza na kuimarisha Ushirikiano wa kikanda wa kushughulikia masuala ya Afya baina ya nchi ya wanachama ikiwemo kutatua changamoto za sekta ya afya, na kupeana uzoefu wa kuboresha huduma za afya.

Mwandishi: Kuni Atley (WAF)

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW