CCM yapitisha wagombea wa nafasi zilizowazi ndani ya chama hicho

Na Dominic Allen

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za mikoa na wilaya zilizokuwa wazi ndani ya CCM pamoja na Jumuiya zake.

Majina ya wagombea hao yamepitishwa kwenye Mkutano huo wa Kamati ya Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM uliyofanyika leo Machi 10, 2025 mkoani Dodoma ambapo Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongoza mkutano huo.

Majina yaliyopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bariadi ni Malongo Lukago Masaba, Mabula Bahati Magamula pamoja na Kitebo Masanja Kulwa.

Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ni pamoja Makamu wa Rais Tanzania, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na viongozi wengine.

Kwa upande wa wilaya ya Liwale, majina ya wagombea watatu yamepitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa wilaya hiyo, ambayo ni Ally Said Jande, Abdallah Ndemane na Salumu Hemedi Titili.

Katika wilaya ya Bagamoyo, majina yaliyopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti kwenye wilaya hiyo ni Latifa Kassim Mwinjuma, Aboubakary Karama Mlawa na Shukuru Halfan Mbatto.

Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM pia imepitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Lindi, ambayo ni Faudhia Abdallah Chiwangu, Kuruthumu Issa Runje pamoja na Asha Abdallah Mahmoud.

Vilevile katika kikao hicho cha leo, majina manne ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya CCM (UVCCM) mkoa wa Singida yamepitishwa, ambayo ni Baraka Mussa Abubakaar, Irene Joseph Malunda, Jumanne Stanlaus Mayunga pamoja na Zulfati Ally Muja.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW