Tanzania yaimarisha mikakati ya Bima ya Afya kwa Wote

Na Dominic Allen

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, hapo jana Februari 05, 2025, amewasilisha mada kuhusu uimarishaji wa mikakati ya Bima ya Afya kwa Wote katika siku ya tatu ya Mkutano wa 156 wa Bodi Tendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) unaoendelea Geneva nchini Uswisi.

Dkt. Magembe amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na WHO katika kutekeleza mikakati yake ya afya kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

Akiainisha hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika kuimarisha afya kwa wote, Dkt. Magembe amesema nchi imetunga na inatekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ili kuwezesha wananchi kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.

Baadhi ya Wajumbe kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania katika Mkutano wa 156 wa Bodi Tendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Geneva nchini Uswisi. Picha: Wizara ya Afya, Tanzania.

Aidha, Tanzania imewekeza kwenye huduma za afya ya msingi, ambapo takriban asilimia 70 ya wananchi wanapata huduma hizo ndani ya umbali wa kilomita tano kutoka wanapoishi.

“Tunazo juhudi za kuwajengea uwezo wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii ili waweze kutambua magonjwa kwa haraka na kuimarisha afua za kinga.” Amesema Dkt. Magembe.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe ameeleza juhudi ambazo zimefanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha utoaji wa huduma za afya hapa nchini.

“Serikali pia imewekeza katika rasilimali watu, vifaa tiba na teknolojia za kisasa kwa lengo la kuboresha huduma za kibingwa na bobezi, kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi ndani ya nchi” amefafanua Dkt. Magembe.

Tanzania inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi wote nchini kwa ufanisi.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW