Ismaili Nyerere, Balozi wa Dwellers Check Hub kutoka jamii ya Wahadzabe, ametoa elimu kwa jamii hiyo kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na mvua za El Niño zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Jamii hiyo imeshauriwa kujenga nyumba imara za asili, ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, katika mafunzo haya yaliyofanyika kuanzia Septemba 24 hadi Oktoba 10, 2026, yakihusisha jumla ya wakazi 300 kutoka vijiji kadhaa, vikiwemo Kaqang’anged, Murus na Mbuga Nyekundu, vilivyopo Kata ya Baray, Tarafa ya Lake Eyasi, mkoani Arusha.

Kwa upande wao, jamii ya Wahadzabe, ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea uwindaji kwa ajili ya kujipatia chakula, imeiomba Serikali na wadau mbalimbali kuwapatia msaada wa maturubai na chakula, wakieleza kuwa mvua hizo zinaweza kuathiri shughuli zao za uwindaji na hivyo kuhatarisha upatikanaji wa chakula na mahitaji yao ya kila siku.
#InternationalMediaSupport #EuropeanUnion #UbaloziwaUswisiTanzania


