Dkt. Samizi ahimiza wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya

Na Wizara ya Afya

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi amewahimiza wananchi kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kula vyakula vyenye lishe bora, kupunguza matumizi ya pombe na bidhaa za tumbaku pamoja na kujenga tabia ya kufanya mazoezi ili kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt. Samizi ametoa wito huo leo Januari 09, 2026 akiwa jijini Arusha wakati akifunga rasmi kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo iliyofanyika katika hospitali ya Arusha, Lutheran Medical Center (ALMC) – Selian, kwa ushirikiano na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

“Kwa niaba ya Waziri wa Afya tunamshukuru kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma za ubingwa na ubobezi za magonjwa ya moyo karibu na wananchi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla,” amesema Dkt. Samizi.

Aidha, Dkt. Samizi ameeleza kuwa kusogezwa kwa huduma hizo mkoani Arusha ni hatua muhimu ikizingatiwa mkoa huo ni kitovu cha utalii na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi akizungumza na wananchi wakati wa kufunga kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo iliyofanyika katika hospitali ya Arusha, Lutheran Medical Center (ALMC) – Selian. (Picha na Wizara ya Afya)

Dkt. Samizi amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa vifo milioni 17.5 sawa na asilimia 32 ya vifo vyote Duniani husababishwa na magonjwa ya moyo, ambapo nchini Tanzania ikiwemo Mkoa wa Arusha una idadi kubwa ya wananchi wanaokabiliwa na ugonjwa huo.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi akisalimiana mmoja wa wananchi katika hospitali ya Arusha, Lutheran Medical Center (ALMC) – Selian. (Picha na Wizara ya Afya)

Ameongeza kuwa magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari na saratani yanaendelea kuleta mzigo mkubwa wa kiafya na kiuchumi kwa jamii, hali inayohitaji jitihada za pamoja za serikali, wadau wa afya na wananchi wenyewe katika kuyazuia na kuyadhibiti magonjwa hayo.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW