Wataalamu PPPC wajadili kilimo biashara na wawekezaji kutoka China

Na Dominic Allen

Wataalamu kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) wakiongozwa na Bw. Dakawa Msoleni Mratibu wa Miradi ya PPP katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa PPP, akiambatana na Bw. David Mushi kutoka Idara ya Miradi, pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya ANHUI HUAFEI INTERNATIONAL TRADES CO. LTD ya China, wamehudhuria kikao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, kujadili fursa za uwekezaji katika kilimo biashara.

Wataalamu kutoka Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), wawekezaji kutoka China pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mkoani Morogoro wakijadili kuhusu fursa zilizopo katika kilimo biashara.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ally Mussa, akiwa ameambatana na Dkt. Rozalia Rwegasira ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji Mali), Bi. Beatrice Njawa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi (Biashara, Viwanda na Uwekezaji), pamoja na viongozi wa Halmashauri za Wilaya ya Mlimba na Malinyi, akiwemo Bw. Filbert Mbwilo na Bw. Geofrey Kamwava.

Katibu Tawala Msaidizi (Biashara, Viwanda na Uwekezaji), Bi. Beatrice Njawa akitoa mchango wake katika kikao hicho maalum kilichowakutanisha wataalamu kutoka Kituo cha PPPC na wawekezaji kutoka China.

Mjadala mkuu katika kikao hicho ulilenga kuibua na kujadili fursa za uwekezaji katika kilimo biashara ndani ya halmashauri hizo mbili, ambapo washiriki walisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kuendeleza miradi ya kilimo, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro.

Mmoja wa wawekezaji wa Kampuni ya ANHUI HUAFEI INTERNATIONAL TRADES CO. LTD akifuatilia mjadala huo uliyojikita katika kujadili kilimo biashara na fursa zilizopo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW