DC Kasongwa aagiza kampuni za ulinzi kukaguliwa

Na Amiri Kilagalila

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe, Kissa Kasongwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya hiyo Mrakibu Mwandamizi, Assel Mwampamba, pamoja na Mshauri wa Jeshi la Akiba kukagua kampuni zote za ulinzi ili kubaini wale wote ambao hawajapitia mafunzo ya Jeshi la Akiba waondolewe.

Ametoa agizo hilo jana Mei 30, 2025 wakati akifungua mafunzo ya mgambo yanayofanyika katika Kata ya Tandala wilayani Makete, ambapo amesema watu wote waliopitia katika mafunzo ndiyo wawekwe kwenye kampuni za ulinzi huku akitaka ukaguzi huo ufanyike ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

“OCD na ofisi yako mfanye ‘vetting’ je, hawa watu wanaolinda wamepitia kwenye mafunzo? Isije kuwa tuna watu wasiokuwa na mafunzo wapo kwenye maeneo nyeti. Lakini fursa yoyote ningependa sana sana sisi kama serikali tuweze kuwafikiria kwanza hawa vijana wenye mafunzo ya jeshi la akiba” amesema DC Kasongwa.

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe, Kissa Kasongwa akizungumza jana Mei 30, 2025 wakati akifungua mafunzo ya mgambo katika Kata ya Tandala Wilayani ya Makete. Picha na Amiri Kilagalila.

“hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, tusome tuyaelewe mafunzo vizuri huku tukitambua amani ndio nguzo yetu ya kwanza katika kuongeza ustawi wa taifa letu lakini tusisahau kuwa wakakamavu” ameongeza DC Kasongwa.

Imani Sanga ambaye ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo ameshukuru, akisema kuwa wapo tayari kwa mafunzo mpaka watakapohitimisha na kuiomba serikali kuwanunulia sare pindi watakapohitimu, jambo ambalo limeungwa mkono na Mkuu wa wilaya, Kissa Kasongwa na kiahidi kuchangia sehemu ya gharama ya mavazi.

“Tunamorali sana na tupo tayari kwa mafunzo na kujenga taifa letu, ila ombi letu tu serikali itusaidie upande wa sare” amesema Sanga.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mgambo wakifuatilia kwa umakini yanayozungumzwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tandala, Altin Sanga amesema kuwa watashirikiana kuona namna ya kuongeza idadi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata Tandala, Daniel Hatanaka ameeleza kuwa mafunzo ya sasa ni ya muda mfupi na yameboreshwa zaidi kuliko kama ilivyokuwa zamani.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW