Dkt. Kahyoza: Ilani ya CCM msingi wa fikra mpya kwenye uchumi wa Tanzania

Na Dominic Allen

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, leo Mei 30, 2025 jijini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano Mkuu Maalum wa chama, amezindua Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2025/2030.

Ilani hiyo mpya imebeba maono ya CCM kwa miaka mingine mitano ijayo, ikimulika vipaumbele tisa ikiwemo kuboresha maisha ya Watanzania, miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia nchini pamoja na vipaumbele vingine ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM ameeleza kuwa Ilani hii imelenga kukuza uchumi jumuishi nchini Tanzania.

“Katika kulinda na kuendeleza mafanikio ambayo jana yameelezwa kwa ustadi mkubwa, lengo kuu la Ilani hii ya uchaguzi wa mwaka 2025 ya CCM ni kukuza uchumi jumuishi na kuimarisha ustawi wa wananchi wote” amesema Prof. Mkumbo.

Wakati Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/2030 ikiwa imejikita kulifikisha Taifa la Tanzania katika nchi ya ahadi, kwa upande Mchambuzi na Mtaalamu wa masuala ya Uchumi, Dkt. Bravious Kahyoza anaona ni wakati sahihi sasa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta mapinduzi ya kiuchumi nchini Tanzania.

“Alipoingia madarakani nilikuwa mtu wa kwanza kusema Rais angeweza kuutengeneza uchumi kwa fikra mpya na nikataja kwamba tunaweza kuwa na Samia-nomics. Kwa hiyo nafikiri wakati huu ndiyo wakati mzuri wa kuona na kupima kinadharia na kivitendo hiyo Samia-nomics” amesema Dkt. Kahyoza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchini (kulia), wote wakiwa wameshikilia Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2025/2030.

Katika siku ya kwanza ya Mkutano Mkuu wa CCM uliyofanyika hapo jana jijini Dodoma, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/2030 imeandaliwa kwa weledi mkubwa.

 “Niwahakikishie kwamba Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu hii tunayokwenda nayo imeandaliwa kwa weledi mkubwa, na kuwashirikisha wananchi wenyewe , Asasi za kiraia, Taasisi za elimu ya juu na wadau wengine wengi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii” alisema Rais Samia.

Dkt. Kahyoza ameitazama Ilani hiyo kwa jicho la kiuchumi akisema kuwa sio tu imelenga kukuza uchumi bali italeta majibu katika kukabiliana na umaskini ambao bado ni janga kwa Watanzania.

“Sio tu ile dhana ya kuongezeka kiuchumi lakini inajaribu kuona ni jinsi gani ukuaji huu utakuwa na majibu ya moja kwa moja kwa Watanzania kwa maana na kukabilana na umaskini” ameeleza Dkt. Kahyoza.

Baadhi ya viongozi pamoja na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliyomalizika leo Mei 30,2025 jijini Dodoma.

Moja ya mambo ambayo yametiliwa mkazo pia katika Ilani hii ni pamoja na kudumisha demokrasia na utawala bora, Dkt. Kahyoza amesema suala la utawala bora litachochea katika kuimarisha uchumi wa Tanzania.

“Suala la utawala bora litakuwa ni sehemu muhimu katika kuimarisha uchumi wa Tanzania kuelekea mbele, na kwa kweli kama ilivyotajwa kwa muda mrefu ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kuimarisha na kujenga uchumi wa kisasa, wakati huo huo ukijaribu kuimarisha suala la utawala bora, kwa sababu wamependekeza kwamba Katiba itaweza kuhuishwa” Dkt. Kahyoza akielezea jinsi utawala bora utakavyochochea kuimarika kwa uchumi nchini Tanzania.

Dkt. Kahyoza ameongeza kuwa ugatuaji wa mitaji kutoka Serikali Kuu kwenda Serikali za Mitaa, ni moja ya mambo ambayo Ilani mpya ya CCM inaenda kuyafanya kwa mustakabali mwema wa Taifa.

“Ni Ilani ambayo inajaribu kufanya ugatuaji wa mitaji kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Serikali za Mitaa, ukiangalia fursa zinarudi kule chini kwa watu” ameeleza Dkt. kahyoza.

Dkt. Kayhoza pia ameungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha utekelezaji wa Ilani hii, ikiwemo kuwepo kwa watu watakaohakikisha inafikia malengo.

“Kama Rais mwenyewe alivyosema kwamba ni lazima kuwepo na watu ambao wanaweza kujibu maswali ya msingi kwenye kutekeleza Ilani hii, na sehemu kubwa sana amesisitiza kupata Wabunge ambao ni wenye maarifa na uwezo wa kusuka Ajenda” maoni ya Dkt. Kahyoza.

Kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025/2030, Dkt. Kahyoza amesema Taifa linaweza kufikia ile dhana ya kubadilisha rasilimali zetu za asili tulizonazo kuwa rasilimali za kiuchumi.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW