TASAF yatoa agizo kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Igomba

Na Amiri Kilagalila

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Peter Ilomo ameipa mwezi mmoja Kamati ya Usimamizi Miradi ya Jamii ya TASAF kijiji cha Igomba kuhakikisha majengo ya zahanati ya kijiji hicho yanakamilika ili iweze kuanza kutoa huduma na kuwapunguzia adha wakazi wa Igomba kufuata huduma ya afya umbali mrefu.

Ilomo ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya zahanati hiyo iliyopo katika kijiji cha Igomba, wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe ambapo amesema uwepo wa zahanati ni muhimu katika kijiji hicho kwa kwani wamekuwa wakifuata huduma ya afya kijiji jirani cha Isimike pamoja na Kituo cha Afya Saja vinavyopatikana umbali wa kilomita 6 kutoka kijijini hapo.

“Tujitahidi usiku na mchana, nimeambiwa mpango ni kumaliza mwezi wa tano lakini na mimi naongeza kidogo mpaka mwezi wa sita kwa kazi nilizoziona ili ikiwezekana mwezi wa saba huduma zianze kutolewa hapa” ameagiza Ilomo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Peter Ilomo (katikati) akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya katika kijiji cha Igomba. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Joyce Mdemwa ambaye ni Mratibu wa TASAF wilaya ya Wanging’ombe amepokea maelekezo ya kukamilisha mradi huo, huku wakazi wa Igomba wakishukuru kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo, kwani itawaondolea changamoto ya kufuata huduma ya afya umbali mrefu.

“Tunatarajia kukamilisha mradi huu tarehe 30/05/2025 na agizo la Mwenyekiti sisi tunamuahidi tutakamilisha na mwezi wa saba tutaanza kutoa huduma” amesema Joyce Mdemwa.

Ujenzi wa Zahanati ya Igomba ukiendelea, ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025. Picha na Amiri Kilagalila.

Kijiji cha Igomba ni miongini mwa vijiji vya wilaya ya Wanging’ombe ambavyo vinanufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) licha ya kusaidia kaya maskini lakini pia kijiji hicho kilipokea Tsh. Milioni 200.2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya zahanati pamoja na nyumba ya mganga.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW