Rais Mwinyi atoa wito kwa Diaspora kuwekeza nchini Tanzania

Na Dominic Allen

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) kuendelea kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini Tanzania pamoja na kuwekeza katika Hati Fungani ya Zanzibar (SUKUK).

Rais Mwinyi ametoa wito huo jana Aprili 06, 2025 akiwa mjini London nchini Uingereza alipokuwa akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini humo, ambapo amesema kuwa serikali inatambua mchango wa Diaspora katika uwekezaji nchini Tanzania pamoja na kuhamasisha utalii hapa nchini.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika ukumbi wa Hoteli ya Capthrone Tara, Uingereza.

Aidha, amewahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa maendeleo ya nchi, huku akiwasisitizia juu ya kuendeleza mila na desturi nzuri za Kitanzania.

Baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza (Diaspora) wakimsikiliza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Katika mkutano huo na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Uingereza (Diaspora), Rais Mwinyi pia amezindua tovuti maalum ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, itakayotoa fursa za kibiashara, uwekezaji, ufadhili wa elimu ya juu pamoja na ajira.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW