Mtandao wa TikTok wazima nchini Marekani

Na Dominic Allen.

Mtandao wa kijamii wa TikTok umesitisha huduma zake nchini Marekani hapo jana kabla ya marufuku ya serikali nchini humo dhidi ya mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya China kuanza kutekelezwa hii leo.

Watumiaji wa mtandao huo maarufu duniani walikutana na ujumbe kutoka TikTok ukisema kuwa “Sheria ya kupiga marufuku TikTok imetekelezwa nchini Marekani. Kwa bahati mbaya, hiyo inamaanisha huwezi kutumia TikTok kwa sasa. Tuna bahati kwamba Rais Trump ameashiria kuwa atashirikiana nasi kutafuta suluhisho la kurejesha TikTok mara tu atakapoingia madarakani. Tafadhali endelea kufuatilia”

Ujumbe huo wa matumaini kutoka kwenye mtandao huo inafuatia baada ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kusema kuwa mara baada ya kuingia madarakani hapo kesho Januari 20, 2025 huenda atatoa msamaha wa siku 90 kwa TikTok dhidi ya marufuku hiyo.

“Kuongeza muda wa siku 90 ni jambo ambalo huenda litafanyika, kwa sababu ni sahihi…nikiamua kufanya hivyo, pengine nitatoa tangazo hilo Jumatatu.” Trump aliliambia shirika la habari la NBC.

Hati hati ya kufungwa kwa TikTok inafuatia sheria iliyotungwa nchini Marekani ambayo imeitaka kampuni ya ByteDance ambayo inamiliki TikTok kuuza mtandao huo kwa kampuni ya Marekani au kufungiwa.

Siku Ijumaa ubalozi wa China nchini Marekani uliishutumu Marekani na kusema kuwa huo ni ukandamizaji na siyo haki kuufungia mtandao wa huo.

Kufungwa kwa TikTok nchini Marekani kutaenda kutaathiri takriban watumiaji milioni 170 nchini humo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW