Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaahidi kuzisimamia vyema Taasisi za Fedha nchini

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda wamekutana na Wakuu wa Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kujadili suala la Hati ya Uwakala katika Ulipaji wa Kodi nchini (Agency Notice).

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salam tarehe 17 Oktoba 2024, Gavana Tutuba amesema lengo la kukutana pamoja kati ya Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mabenki na Taasisi za Fedha ni kuona namna wanavyoweza kuboresha utendaji wa kazi kwa kushirikiana na kuweka mazingira rafiki ya biashara kwa wananchi bila vikwazo vyovyote.

Bw. Tutuba amesema Benki Kuu ya Tanzania itahakikisha inasimamia vyema Taasisi za Fedha na kutatua changamoto zilizopo ili wanaotakiwa kulipa kodi walipe bila kushurutishwa kama Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoagiza.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu Mwenda amesema kuwa Hati za Uwakala ni njia ya mwisho kabisa ya kukusanya kodi na TRA itaendelea kutoa elimu na kujenga mahusiano ya karibu zaidi na walipakodi ili waweze kulipa kodi zao kwa wakati kwa lengo la kuondokana na matumizi ya Hati hizo za uwakala katika Ulipaji wa Kodi.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW