Watumishi wa afya wapewa wito kubeba ujuzi kutoka kwa Madaktari Bingwa

Na Amiri Kilagalila

Serikali mkoani Njombe imetoa wito kwa watumishi wa afya wa mkoa huo kujitoa na kufanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Madaktari Bingwa waliofika mkoani humo kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa, ili kupata ujuzi kutoka kwa madaktari hao.

Wito huo umetolewa leo Mei 26, 2025 na Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Judica Omary mara baada ya kupokea timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia inayozunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa.

“Tuna hospitali kila halmashauri lakini pia vifaa tiba vimekuja kwa wingi kiasi kwamba unakuta watumishi wengine inabidi wajifunze jinsi ya kutumia, kwa hiyo tunawaombeni sana mjitoe katika kuwaelewesha watumishi wetu namna bora ya kutumia vifaa, ili hata mtakapokuwa mnaondoka mtakuwa mmewaacha watu wanaoendeleza kazi kwa ubora” amesema Judica Omary.

Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Judica Omary leo Mei 26, 2025 akizungumza na baadhi ya watumishi wa afya wa mkoa wa Njombe wakati wa mapokezi ya timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia. Picha na Amiri Kilagalila.

Nae Dkt. Robert Masele ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Njombe amesema mkoa huo umeendelea kunufaika na timu ya Madaktari Bingwa ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi wa afya ambapo kwa sasa wamefanikiwa kupokea jumla ya madaktari 38 watakaokwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Njombe.

“Mkoa wa Njombe tumekuwa tukinufaika sana na Madaktari Bingwa, na maeneo ambayo yamekuwa yakitupa changamoto sana ni eneo la afya ya uzazi na magonjwa ya watoto, ambapo timu hii imekuwa ikitusaidia na tumepokea jumla ya madaktari 38 ambao watafanya kazi kwa siku sita” amesema Dkt. Robert.

Katibu Tawala mkoa wa Njombe, Judica Omary (wa tatu kutoka kulia) pamoja na Mratibu wa zoezi la Madaktari Bingwa mkoa wa Njombe, Paskalina Andrew (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia. Picha na Amiri Kilagalila.

Kwa upande wake, Paskalina Andrew ambaye ni mratibu wa zoezi la Madaktari Bingwa awamu ya tatu kwa mkoa wa Njombe akitokea Wizara ya Afya katika Idara ya afya uzazi mama na mtoto, ameeleza kuwa lengo lao ni kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi ili kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.

“Zoezi hili la kutoa huduma za kibingwa linaanza leo tarehe 26 mpaka tarehe 31 na lengo letu ni kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa bobezi karibu na wananchi ambapo itawarahisishia kutosafiri umbali mrefu kufuata huduma” amesema Paskalina Andrew.

Mratibu wa zoezi la Madaktari Bingwa awamu ya tatu kwa mkoa wa Njombe, Paskalina Andrew akitoa ratiba ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia waliofika mkoani humo kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya madaktari waliofika mkoani Njombe, Dkt James Msigwa ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya pua, maskio pamoja na koo amesema kuwa katika siku sita watakazokuwepo mkoani Njombe wana matarajio makubwa ya kutoa huduma bora kwa wananchi wengi watakaokutana nao.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW