UWT: Wanaoondoka CHADEMA tunawakaribisha

Na Amiri Kilagalila

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe, Dkt. Scholastika Kevela amesema kuwa viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Njombe waliojiondoa katika chama hicho, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinawakaribisha, ambapo amesema kuwa chama chao wanao utaratibu wa kusikilizana.

Dkt. Kevela ameeleza hayo hapo jana mjini Njombe wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Njombe, ambapo Kamati ya Utekelezaji ya UWT mkoa wa Njombe imekutana na viongozi wao kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama na jumuiya.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Njombe walioshiriki katika kikao kilichofanyika mjini Njombe jana Mei 17, 2025 ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya CCM na UWT.

“Nimesikia Njombe pia wanagawana vilago,sisi tunawakaribisha milango iko wazi ila wasije na vurugu, Chama cha Mapinduzi (CCM) tunasikilizana kwa hiyo yakiwashinda huko njoeni” amesema Dkt. Kevela.

Kauli ya Dkt. Kevela inafuatia baada ya baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA mkoani Njombe akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mkoa wa Njombe, Veronica Mlonganile,Patrick Njulumi ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Wanging’ombe, Lea Masasi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Jimbo la Lupembe pamoja na wanachama wengine ishirini kujivua uanachama jana Mei 17, 2025.

Licha ya viongozi hao pamoja na wanachama wa CHADEMA licha ya kuondoka kwenye chama hicho, walisema kuwa bado wataendelea kufanya siasa na kuwasemea wananchi changamoto zao katika majukwaa mengine.

Wakati baadhi ya viongozi pamoja na wanachama wa CHADEMA wakiendelea kuondoka kwenye chama hicho, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika mnamo Mei 16, 2025 akiwa Maswa mkoani Simiyu katika mkutano wa hadhara alitoa maelekezo kwa viongozi wa chama hicho kurejea kwenye mwongozo wa katiba ya chama ili kuziba nafasi za viongozi wa chama ambao wameamua kuondoka.

Katika mkutano huo, Mnyika alisema kuwa pindi baadhi ya viongozi wa chama wanapoamua kusaliti mapambano na kuondoka CHADEMA, viongozi pamoja na wanachama waliosalia katika maeneo husika wanapaswa kutumia katiba ya chama kuziba nafasi hizo ili kuendeleza mapambano.

Mwandishi: Amiri Kilagalila

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW