Wakili Amsterdam atoa wito kwa Jamii ya Kimataifa kuingilia kati sakata la Lissu

Na Dominic Allen

Wakili wa Kimataifa, Robert Amsterdam ambaye anamwakilisha Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu amelaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi Tanzania kumkamata Tundu Lissu na kumfungulia mashtaka ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, ambapo amesema kuwa Jeshi la Polisi limekiuka haki za binadamu na wala halikufuata sheria.

Wakili Amsterdam amezungumza hayo jana Aprili 10, 2025 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinaharibu taswira ya Tanzania na maslahi ya wananchi wote kwa ujumla.

“Hakukuwa na vitendo vyovyote vya vurugu, hakuna msingi wa kukamatwa, wala taratibu za kisheria zilizofuatwa” akielezea Wakili Amsterdam juu ukamataji uliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Tundu Lissu hapo jana akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili. Picha na Mwl. John Pambalu.

Wakili Amsterdam amesema Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatumia mamlaka yake kuwanyamazisha wakosoaji wake, akiongeza kuwa tangu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi mnamo mwaka 2017, ameendelea kukumbana na vitendo vya kukamatwa mara kwa mara na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kisiasa.

“Katiba ya Tanzania inahakikisha haki ya uhuru wa kujieleza, kuungana, kusafiri na kushiriki katika siasa – haki zote hizo kwa sasa zinakiukwa” imesema taarifa ya Wakili Amsterdam.

Wakili Robert Amsterdam ametoa wito kwa Jamii ya Kimataifa kuingilia kati suala hilo na kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Tundu Lissu (Kushoto) akiwa na Wakili Robert Amsterdam (Kulia) mjini Brussels, Ubelgiji.
Picha na Tundu Lissu.

Tundu Lissu na baadhi ya viongozi wengine pamoja na wanachama wa CHADEMA walikamatwa na Jeshi la Polisi Aprili 09, 2025 wakiwa Mbinga mkoani Ruvuma mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara, ambapo wengine aliokamatwa nao waliachiwa huru, lakini yeye alisafirishwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, na jana Aprili 10, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, alifunguliwa mashtaka mawili ambayo ni uhaini pamoja na kutoa taarifa za uongo.

Hata hivyo, Mahakama ilihairisha kesi ya uhaini hadi Aprili 24, 2025 kwa kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo. Katika shtaka la pili, Lissu anakabiliwa na makosa matatu ya kutoa taarifa za uongo, Lissu amekana makosa yote ya shtaka la pili, kesi hiyo pia itasikilizwa tena Aprili 24, 2025.

Ijapokuwa shtaka la pili linadhamika, lakini Mahakama haikumuachia huru Tundu Lissu kutokana na shtaka la kosa la uhaini linalomkabili.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW