Samia Scholarship kutoa kipaumbele kwa watumishi wa vituo vya afya ngazi ya msingi

Na Wizara ya Afya

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe kutoa kipaumbele kwa watumishi kutoka vituo vya afya ngazi ya msingi kwa kuwapeleka kusoma utaalam wa kibingwa na ubobezi kupitia mfuko wa Samia Scholarship, ili kuendelea kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi.

Waziri Mhagama ameyasema hayo Aprili 09, 2025 wakati wa kufunga Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.

“Rais Dkt. Samia ametoa mfuko maalum wa kusomesha wataalam katika sekta ya afya ujulikanao kama Samia Scholarship, hivyo ni lazima tusomeshe kwa seti yaani daktari, mtaalamu wa usingizi, mtaalam wa maabara, na wauguzi tusiwaache nyuma, hivyo tunapoamua kuwapeleka watumishi wa afya kusoma hawa watumishi kutoka vituo vya afya vya msingi wapewe kipaumbele kwa sababu hawa ndio wanaotoa huduma ya matibabu kwa asilimia 80, hivyo ni vyema kupeleka huduma za kibingwa na bobezi ngazi ya msingi” amesema Mhagama.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi. Picha na Wizara ya Afya.

Waziri Mhagama amewataka waganga wafawidhi kuwa mfano wa kuigwa kwa maadili mema na kuwasimamia vizuri watumishi wanaowaongoza ili kuhakikisha kwa pamoja sekta ya Afya inapata heshima kwa kufuata viapo walivyoapa, miongozo na maadili.

“Niwaombe sana Waganga Wafawidhi kusimamia mifumo ya matumizi, usimamizi na uendeshaji wa vituo vya afya ngazi ya msingi hasa wa mapato” amesema Waziri Mhagama.

Ameongeza kuwa Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tamisemi wako mbioni kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kugawa vishikwambi 600 na kwa waganga wafawidhi ili kuendana na kasi ya ulimwengu wa kidijitali.

Aidha, Waziri Mhagama amesema Wizara ya Afya inatekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kupeleka kiasi cha Tsh. Bilioni 1 Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kusaidia kufikisha mfumo wa usimamizi katika maeneno ambayo haujafika.

Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW