Bashungwa awataka Maafisa Uhamiaji kujiepusha na rushwa

Na Dominic Allen

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewataka Maafisa na Askari wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwasihi kuepukana na vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea wahamiaji haramu kuingia nchini.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo jana Machi 04, 2025 wilayani Karagwe, mkoani Kagera wakati akizungumza katika Kikao Kazi na Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

“Wizara itawasimamia kikamilifu Maafisa Uhamiaji katika kutekeleza majukumu yao, wale ambao watakosa uzalendo na uadilifu na kuwa sehemu ya chanzo cha kuchochea uingiaji wa wahamiaji haramu kwa lengo la kujipatia fedha au rushwa, watachukuliwa hatua kali za kisheria” alisema Bashungwa.

Baadhi ya washiriki katika Kikao Kazi kilichofanyika Machi 04, 2025 wilayani Karagwe mkoani Kagera, ambacho kiliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa. Picha na Wizara.

Waziri Bashungwa ameongeza kuwa mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ambayo ipo mipakani inayokumbwa na changamoto ya wageni kutoka nchi jirani kuingia nchini kinyume na taratibu kutokana na ukubwa wa mipaka.

Hata hivyo ametoa wito kwa viongozi wa vijiji, kata na wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Maafisa wa Uhamiaji ili kukomesha uingiaji wa wahamiaji haramu nchini.

Vile vile Waziri Innocent Bashungwa amewataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka pindi wanapoona Maafisa wa Uhamiaji wanajihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili, ikiwemo rushwa ili kuhakikisha kila mgeni anayeingia nchini anaingia kwa mujibu wa sheria.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW