Bashe: Malawi yazuia mazao ya kilimo kutoka Tanzania kuingia nchini humo

Na Dominic Allen

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa serikali imepokea taarifa rasmi kuwa Serikali ya Malawi imezuia kuingia kwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania, yakiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi pamoja na mahindi, jambo ambalo limeathiri moja kwa moja shughuli za wafanyabiashara wa Tanzania wanaosafirisha bidhaa hizo kwenda Malawi.

Waziri Bashe amebainisha hayo leo Aprili 17, 2025 kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, ambapo amesema kwa kipindi cha miaka mitano Serikali ya Tanzania pia imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kufungua soko la ndizi Afrika ya Kusini bila mafanikio.

“Ni vyema ifahamike kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio. Hali hii inafanana na changamoto tulizopitia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale tulipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi yetu.” Amesema Waziri Bashe.

Kufuatia zuio hilo la Malawi baada ya kushindikana kwa juhudi zote za kidiplomasia, Bashe amesema iwapo Malawi na Afrika Kusini hazitabadili misimamo yao, Tanzania itazuia uingizwaji wa bidhaa zote za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini.

“Iwapo Serikali ya Malawi na Afrika Kusini hazitabadilisha msimamo wao kufikia Jumatano ijayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili.” Ametoa msimamo huo Waziri Bashe.

Vilevile Waziri Hussein Bashe ameongeza kuwa mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini hazitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi pale zuio hilo litakapoondolewa.

Katika kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania, pia usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa.

Hata hivyo, Bashe ametoa wito kwa wasafirishaji wote wa Kitanzania wanaosafirisha bidhaa za kilimo kuacha kupakia bidhaa hizo mpaka hapo Malawi na Afrika Kusini watakapobadilisha misimamo yao.

“Wafanyabiashara walioweka order za apples, machungwa na bidhaa zingine ambazo hununuliwa Afrika kusini, ninawashauri kuacha kwa sasa kwani hatutoziruhusu kuingia Tanzania mpaka hapo Afrika Kusini itakapo tufungulia soko la ndizi.” Amesisitiza Bashe.

“Ninathibitisha kuwa kama Waziri mwenye dhamana, nimewasiliana kwa njia mbalimbali na Waziri wa Kilimo wa Malawi bila mafanikio ya kupata majibu rasmi.” Ameongeza Bashe.

Waziri Hussein Bashe amesema hatua hizo zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania zimelenga kulinda heshima ya nchi, uchumi wa wakulima nchini pamoja na usawa katika biashara za kikanda.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW