Mwanaharakati aliyetoweka nchini Kenya, mwili wake wakutwa mochwari

Na Dominic Allen

Mwili wa mwanaharakati nchini Kenya, Ibrahim Hilal Mwiti aliyetoweka tangu mwezi Novemba, 2024 wakutwa mochwari katika Hospitali ya Thika nchini humo.

Kabla ya kutoweka kwake, Mwiti alionekana kwa mara ya mwisho jijini Nairobi, ambapo wanafamilia na marafiki walianza juhudi za kumtafuta kupitia hata kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo Novemba 15, 2024 ndugu wa mwanaharakati huyo walifungua jarida la kutoweka kwake Na. 80A/13/11/24 katika Kituo cha Polisi Kamukunji.

Familia ya Mwiti baada ya kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio, walifanya maamuzi ya kuangalia kwenye mochwari ambapo Januari 02, 2025 waliupata mwili wake.

Kwa mujibu wa mama yake Mwiti, Sadhiya Iman wakati wa mazishi ya mwanae katika makaburi ya Lang’ata amesema walijulishwa kuwa mwanae alifariki baada ya kugongwa na gari, ambapo waliomgonga walikimbia.

Hata hivyo familia yake imezitaka mamlaka nchini Kenya kuchunguza kwa undani juu ya kifo cha Mwiti na kuja na majibu ya kueleweka.

Mpaka sasa mamlaka nchini Kenya hazijazungumza chochote kuhusiana kifo cha mwanaharakati huyo, ambaye amepoteza maisha katika kipindi ambacho kumekuwa na matukio ya utekaji wa wanaharakati huku baadhi ya maafisa Jeshi la Polisi la Kenya wakihusishwa na matukio hayo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW