Kampuni ya Adani ya India inakabiliwa na shutuma za ubaguzi wa rangi katika kitengo chake cha makaa ya mawe cha Australia baada ya wanachama wa kundi la wenyeji Australia kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Haki za Kibinadamu nchini humo.
Wafanyakazi wa Adani wanatuhumiwa kutoa lugha kali na kuwazuia wanachama wa kundi la wenyeji wa Australia kwenda kwenye vyanzo vya maji karibu na mgodi wa makaa ya mawe wa Carmichael wa Adani ili kutekeleza ibada zao kitamaduni.
Tuhuma hizo zinafuatia baada ya Mwenyekiti wa kampuni hiyo bilionea Gautam Adani na wengine saba kufunguliwa mashtaka mjini New York, Marekani kwa tuhuma kutoa rushwa ya dola za Kimarekani milioni 265 kwa maafisa wa serikali ya India ili kupata mikataba ambayo ingeleta faida ya dola za Kimarekani bilioni 2 katika kipindi cha miaka 20.
Mahakama mjini New York ilishatoa hati za kukamatwa kwa Gautam Adani na mpwa wake Sagar Adani na waendesha mashtaka wanapanga kukabidhi hati hizo kwa vyombo vya sheria vya kigeni.


