BOT: Akiba ya Dhahabu fedha sasa ni USD milioni 30.32

Na Yohani Gwangway

Mafanikio Yaliyopatikana Jul 2023– Nov 2024

Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Anna Lyimo amesema kuwa benki hiyo imeongeza akiba ya dhahabu fedha yenye thamani kutoka dola za kimarekani milioni 23 hadi dola za kimarekani milioni 30.32 kati ya kipindi cha mwezi Julai mwaka 2023 hadi mwezi Novemba mwaka huu, ambapo kwa sasa hivi BOT ina akiba ya dhahabu fedha kilogramu 366.55.

Dr. Lyimo amesema kuwa kwa upande mwingine akiba ya Benki Kuu ya Tanzania katika manunuzi ya dhahabu safi imefikia  kilogramu  872.05 zenye thamani ya dola za kimarekani milioni  74.04. Manunuzi haya ni kutoka kwa wauzaji mbalimbali pamoja na masoko ya dhahabu nchini Tanzania ambayo yananunua dhahabu kutoka kwenye viwanda vya uchenjuaji dhahabu.

Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Anna Lyimo akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa Benki Kuu kuwa na akiba ya Dhahabu Fedha, Novemba 14, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya BOT mafanikio yao katika kununua dhahabu na kuweka akiba ni kutokana na jitihada mbalimbali zilizowekwa na serikali ikiwa ni pamoja na punguzo la malipo ya mrabaha kutoka 6% mpaka 4% kama inavyolipwa kwa wauzaji kwenye viwanda vya kuchenjulia dhahabu nchini. Sababu nyingine ni kununua dhahabu inayotokana na malipo ya 1/3 ya malipo ya mrabaha pamoja na dividends yanayotarajiwa kulipwa (in kind) kwa mujibu wa sheria.

Kwa sasa Benki Kuu ya Tanzania inapata urahisi wa kununua dhahabu zake kutoka kwa wachimbaji wakubwa pamoja na wadogo kutokana na mabadiliko na maboresho katika Sekta ya Madini kati ya mwaka 2018 na 2019.

“Mwaka 2018-2019 tunafahamu kuwa serikali ilifanya mabadiliko makubwa sana kwenye Sekta ya Madini na wakaanzisha viwanda vya kuchenjua dhahabu kwa hiyo sasa hivi dhahabu tukinunua tuna mtu ambaye anaenda kutupimia na siyo sisi tena”. Aliongeza Dkt. Lyimo.

Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuanza kununua dhahabu kwa mara nyingine tena baada ya kile kipindi cha mwaka 1990 hadi mwaka 2003 ambapo walisitisha kutokana na changamoto mbalimbali ili kuimarisha akiba yake ya fedha za kigeni na kupunguza utegemezi Tanzania kwa mataifa ya nje.

Maamuzi ya Benki Kuu ya Tanzania kununua dhahabu kwa mara nyingine yameanza mwaka 2022 huku Dkt. Lyimo akieleza kuwa haya ni maamuzi ya busara kwa taifa letu. Mataifa mengi yameanza kununua dhahabu na kuweka kama akiba hasa baada ya mwaka 2010 ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kutokea kwa mtikisiko wa Uchumi Duniani ulioathiri mataifa mbalimbali.

“Ina maana kuna kitu kimetokea hapa, dunia ikabadilisha mtazamo na kufanya manunuzi ya dhahabu yatoke chini na kupanda juu. Kilichotokea baada ya mtikisiko wa uchumi duniani (Global Financial Crisis) ni kuwa nchi zote duniani ziligundua kuwa ukikaa na pesa kama pesa, bado haujapona, pale ndiyo wakarudi katika manunuzi ya dhahabu”. Alifafanua Dkt. Lyimo.

Historia ya ununuzi wa dhahabu kama akiba ya fedha za kigeni imeonesha mfanano wa muda mrefu.  Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa kila thamani ya dola ya Marekani inaposhuka, thamani ya dhahabu huimarika katika soko la dunia na wakati thamani ya dola inapopanda, dhahabu hushuka thamani. Licha ya matukio haya, Dkt. Lyimo anaeleza kuwa ununuzi wa dhahabu ndiyo njia imara ya kuwa na pesa za kigeni pamoja na kuimarisha thamani ya pesa zetu.

Benki Kuu ya Tanzania inatoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari takribani 36 kutoka mikoa 6 yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuandika habari za kifedha na kiuchumi.

Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya siku mbili yanayotolewa na Benki ya Tanzania ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuandika habari za kifedha na kiuchumi kwa weledi.

Faida za Benki kununua dhahabu ni kama zifuatazo;

  • Kuimarisha akiba ya fedha za kigeni kwa taifa na kupunguza utegemezi wa nje.
  • Kutoa kiwango cha kujiamini kuhusu hali ya kifedha.
  • Kuweka soko la kuvutia kwa wasambazaji wa dhahabu wa ndani.
  • Kuonesha uthabiti wa sarafu ya ndani.
  • Kusaidia kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni na deni la nje.
  • Kuhifadhi akiba kwa ajili ya majanga au dharura za kitaifa.
  • Kutumia rasilimali yetu ya dhahabu kwa manufaa ya kiuchumi.

Mwandishi: Yohani Gwangway
Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW