BIBI CARE wazindua Kampeni ya ‘WASITIRI’

Na Edward Kinabo

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bi. Fatma Mwassa, amezindua kampeni ya ‘WASITIRI’ inayolenga kutoa elimu ya hedhi salama na kuhamasisha upatikanaji wa taulo za hedhi kwa ajili ya kuwasitiri maelfu ya wanafunzi wasichana nchini, ikianzia mkoa wa Kagera.

Kampeni hiyo inayotekelezwa na Shirika la BIBI CARE kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ilizinduliwa Oktoba 19, 2024 katika ukumbi wa KCU, mjini Bukoba katika tamasha la Huruma ya Mungu lililosheheni burudani ya  kwaya mbalimbali kutoka nchini na nchi jirani ya Uganda.

Akizindua kampeni hiyo, Bi Mwassa alisema uhitaji wa taulo za kike ni mkubwa kuliko inavyofikiriwa, kwani yeye binafsi aliwahi kufanya kampeni iliyotoa misaada ya shuka, vyandarua, sare za shule, viatu vya ngozi, soksi, madaftari, kalamu na taulo za kike kwa wasichana wa shule za bweni, lakini alipowarudia kuhoji wamefurahia nini zaidi, wanafunzi wengi walitaja taulo za kike.

“Yaani umempa binti shuka mbili, chandarau, sare za shule, viatu vya ngozi, soksi, madaftari na kalamu, lakini anakwambia amefurahia zaidi taulo za kike. Hii inaashiria kwamba uhitaji wa taulo za kike ni mkubwa zaidi kuliko tunavyofikiria,” alisema Bi Mwassa.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bi. Fatma Mwassa akihutubia wakazikatika uzinduzi wa Kampeni ya ‘WASITIRI’ ya Shirika la BIBI CARE iliyofanyika Oktoba 19, 2024.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bi. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la BIBI CARE, Edward Kinabo (kulia) pamoja na washiriki wengine.

Awali, Mwenyekiti wa BIBI CARE, Edward Kinabo, alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘WASITIRI’ shirika hilo pamoja na wadau wake, wamejipanga kutoa elimu na kusaidia taulo za kike kwa wanafunzi ili kupunguza tatizo la baadhi yao kukosa masomo kwa sababu ya kushindwa kujisitiri wakati wa hedhi.

Ameongeza kuwa utafiti wa UNICEF uliofanyika kwenye wilaya 19 nchini ulithibitisha kuwa asilimia 16.8 ya wanafunzi wa kike wanakosa masomo wakiwa katika siku zao za hedhi, huku akiweka angalizo kuwa kama ukifanyika utafiti mpana zaidi wa ngazi ya taifa basi huenda tatizo hilo likaonekana kuwa kubwa zaidi kuliko lilivyoonekana kwenye wilaya 19 zilizofanyiwa tafiti.

Mwenyekiti wa Shirika la BIBI CARE, Edward Kinabo, akizungumza wakazi wa mji wa Bukoba Oktoba 19, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘WASITIRI’ inayotekelezwa na shirika hilo.

Akigusia awamu ya pili ya kampeni hiyo, Kinabo amesema ili kuhakikisha upatikanaji endelevu na nafuu wa taulo za kike, BIBI CARE imejipanga kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana kumiliki na kuendesha viwanda vidogo vya kuzalisha taulo za kike za kutengenezwa kwa kutumia nyuzi za mgomba.

“Kagera mnalima ndizi. Tunakwenda kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Taulo za kike za mgomba zitaleta fursa ya kutengeneza vipato kwa wakulima wa zao la ndizi na wakati huo huo tutakuwa tumechangia upatikanaji endelevu na nafuu wa taulo za kike. Tutahakikisha taulo hizo zinakidhi viwango vya ubora na kupata ithibati ya TBS,” alisema Kinabo.

Utekelezaji wa Kampeni ya ‘WASITIRI’ inayosimamiwa na Shirika la BIBI CARE inatarajiwa kuleta matokeo chanya yaliyo endelevu kwa jamii.

Mwandishi: Edward Kinabo
Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW