Wananchi Ngorongoro walalamikia NCAA kukamata mifugo na wafugaji Ndutu

Baadhi ya wakazi kutoka kata ya Endulen, tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha, wameituhumu Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kukamata mifugo yao pamoja na wao wenyewe katika eneo la Ndutu, jambo ambalo wamedai kuwa ni kinyume na makubaliano yaliyopo kati ya jamii na mamlaka hiyo ya hifadhi.

Kwa mujibu wa wananchi hao, akiwemo Joseph kutoka kijiji cha Nasipaoriong, wamesema utaratibu uliopo ni kuwa kuanzia mwezi wa 12 hadi wa 5, wafugaji husitisha kupeleka mifugo kwenye eneo la Ndutu kwa ajili ya kupisha shughuli za utalii pamoja na uhamaji wa nyumbu, huku wakitakiwa kuwa huru kupeleka mifugo baada ya kipindi hicho kupita, lakini makubaliano hayo kuhusiana na suala la malisho katika eneo hilo bado limeendelea kuwa changamoto.

Kufuatia malalamiko hayo, Land Dwellers imemtafuta Kaimu Meneja  Uhusiano wa Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Hamis Dambaya, ambapo ameeleza hana taarifa juu ya kukamatwa kwa mifugo na watu katika eneo la Ndutu, licha ya wananchi hao kubainisha kuwa wamekuwa na changamoto hiyo kwa takribani miaka minne sasa.

#Hakizawafugaji #Hakizaardhi #Jamiizaasili #Ndutu

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW