Zaidi ya ng’ombe 479,800, kuku milioni 2.3 kupatiwa chanjo, Songwe

Na Dominic Allen

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezindua rasmi programu ya kitaifa ya utoaji wa chanjo na utambuzi wa mifugo kwa mkoa wa Songwe, ambapo zaidi ya ng’ombe 479,800 na kuku zaidi ya milioni 2.3 wanatarajiwa kupatiwa chanjo.

Programu hii ambayo katika ngazi ya mkoa imezinduliwa jana Julai 7, 2025, katika Kijiji cha Ndanga, Kata ya Mbuyuni, Wilaya ya Songwe ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo kwa Mifugo iliyoanzishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, akiongoza uzinduzi huo, amesema kuwa programu hiyo imelenga kukinga mifugo dhidi ya homa ya mapafu ya ng’ombe na kwa upande wa kuku ni kideri, ndui pamoja na mafua, ambapo chanjo hizo zote zimepata ruzuku kutoka Serikali ili kuwasaidia wafugaji kupata huduma hiyo.

“Katika siku ya kwanza ya uzinduzi, zaidi ya ng’ombe 1,500 wamechanjwa na kutambuliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songwe,” alisema Dkt. Mhede.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede (kushoto) akiongoza zoezi la uvishaji hereni kwa Ng’ombe alipotembelea wafugaji wa mkoa wa Songwe Julai 07, 2025, ikiwa ni muendelezo wa zoezi la uhamasishaji utoaji chanjo na utambuzi wa mifugo liliyofanyika katika kijiji cha Ndanga, wilaya ya Songwe, mkoani Songwe.

Dkt. Mhede ameongeza kuwa Serikali imeamua kuwawezesha wafugaji nchini kwa kutoa ruzuku kwenye zoezi hili, ambapo kwa sasa watachangia kiasi cha Shilingi za Kitanzania 500 tu kwa chanjo ya ng’ombe mmoja badala ya Shilingi za Kitanzania 1,000, huku kuku wakichanjwa bure.

Aidha, mpango huu wa Serikali pia umelenga kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, kwani baada ya kupatiwa chanjo na kutambuliwa, wafugaji wataweza kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha na kushiriki kwenye biashara ya kimataifa.

Kupitia utekelezaji wa zoezi la chanjo na utambuzi wa mifugo, mara baada ya kuchanjwa, mifugo hiyo itatambuliwa kwa kuvishwa hereni za kielektroniki ambazo zitasaidia utambuzi wa haraka endapo mnyama atapotea au kuibiwa.

Kwa upande wake, Mshauri wa Mifugo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Ayubu Rajabu, amesema kuwa mkoa umeanza kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa chanjo na utambuzi wa mifugo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 05, 2025 na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo kwa mwaka 2024/2025 inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2025, ambapo zaidi ya mifugo milioni 70 itachanjwa nchi nzima kukingwa dhidi ya magonjwa yanayoathiri biashara ya mifugo na mazao yake.

Mwandishi: Dominic Allen
Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW