Amnesty International yasema Jeshi la Polisi Msumbiji lilikiuka haki za binadamu wakati wa maandamano

Na Dominic Allen

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetaka uchunguzi wa kina ufanyike kufuatia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliyofanywa na vyombo vya usalama nchini Msumbiji wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 09, 2024.

Amnesty International wamebainisha ukiukwaji huo wa haki za binadamu katika ripoti yao mpya waliyotoa jana Aprili 15, 2025 yenye jina Maandamano yashambuliwa: Ukiukwaji wa haki za binadamu baada ya uchaguzi wa 2024 nchini Msumbiji.

Katika ripoti hiyo, Amnesty International kupitia vyanzo vya wazi na mahojiano, wamepata ushahidi kuwa vyombo vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi walitumia nguvu zisizo za lazima na pasipo kujali dhidi ya waandamanaji waliyokuwa wakiandamana kwa amani.“Silaha za moto siyo zana ya kimkakati ya kudhibiti mikusanyiko ya umma” imesema ripoti hiyo.

“Ripoti ya Amnesty International imetokana na video na picha 105 zilizothibitishwa, pamoja na mapitio ya taarifa nyingine kutoka vyanzo vya wazi na mahojiano 28, wengi wa wakiwa ni mashahidi na waathirika kati ya Oktoba 2024 na Januari 2025” imesema taarifa ya shirika hilo ikielezea kuhusu ripoti hiyo.

Mwandamanaji akitupa jiwe wakati wa mgomo wa kitaifa uliyoitishwa na mgombea urais wa Msumbiji, Venâncio Mondlane, kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 09, 2024. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko.

Jeshi la Polisi nchini Msumbiji walihusika kuua takriban watu 400 katika kipindi cha miezi mitatu ya ukandamizaji dhidi ya maandamano ya upinzani, limesema shirika la Amnesty International, likilaani vikali matumizi ya nguvu kupita kiasi na ukosefu wa uwajibikaji.

Hapo jana, Naibu Mkurugenzi wa Kanda wa Amnesty International kwa Afrika Mashariki na Kusini, Khanyo Farise ametoa wito kwa Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo kufanya uchunguzi wa kina juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliyotokea wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Msumbiji mwaka jana.

“Iwapo serikali mpya ya Rais Daniel Chapo inataka kufungua ukurasa mpya, ni lazima ihakikishe kuwa kuna uchunguzi wa kina na wa wazi kuhusu tuhuma zote za ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa ukandamizaji huo, na kuwawajibisha wote wanaoshukiwa kuhusika” alisema Khanyo Farise.

Waandamanaji jijini Maputo, Msumbiji wakiwa wamebeba jeneza lenye uso wa Daniel Chapo wa chama cha FRELIMO. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko.

Amnesty International imelitaka Jeshi la Polisi nchini Msumbiji kutotumia silaha za moto kutawanya waandamanaji wa amani, huku ikisisitiza kuwa matumizi ya silaha hizo yawe pale itakapowalazimu dhidi ya mtu ambaye ni tishio au anahatarisha maisha.

“Kuhakikisha kuwa silaha za moto hazitumiki kutawanya mikusanyiko, na kwamba zinatumika tu kujibu tishio la kifo au majeraha makubwa, na zinatumika mahsusi dhidi ya mtu anayetoa tishio hilo na si kufyatuliwa kiholela kwa umati wa watu” imesema ripoti hiyo ikilitaka Jeshi la Polisi kuwa makini katika matumizi ya silaha za moto.

Licha ya ripoti hiyo ya Amnesty International, mamlaka nchini Msumbiji hazijasema chochote hadi sasa kuhusiana na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu uliyofanywa na vyombo vya usalama nchini humo.

Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi nchini Msumbiji yalizuka Oktoba 21, 2024 baada ya kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba 09, 2024 ambapo chama cha upinzani cha PODEMOS na mgombea wake, Venâncio Mondlane walidai kuwa kulikuwa na wizi wa kura kwa manufaa ya chama tawala cha FRELIMO na mgombea wake, Daniel Chapo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW