Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Jamhuri

Na Dominic Allen

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Oktoba 13, 2025 imetoa uamuzi mdogo katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, kufuatia pingamizi lililokuwa limewekwa na Mawakili wa upande wa Jamhuri.

Juma lililopita upande wa Jamhuri uliweka pingamizi baada ya Lissu kuomba kielelezo D1, ambayo ni maelezo ya maandishi ya shahidi wa pili wa Jamhuri, Inspekta wa Jeshi la Polisi, John Kaaya aliyoandika akiwa kwenye Kituo cha Polisi. Mawakili wa upande wa Jamhuri ulipinga ombi hilo kwa madai kuwa mshtakiwa hakuzingatia taratibu za kisheria katika kuomba kielelezo hicho.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umefuatia baada ya Jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, wamesema kuwa mshtakiwa ambaye ni Tundu Lissu amefuata taratibu zote zinazohitajika kisheria katika kuomba kielelezo hicho kupokelewa Mahakamani.

Baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali pingamizi hilo la upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ambayo inaendelea leo, kielelezo hicho kinakuwa cha kwanza cha mshtakiwa kuwasilishwa Mahakamani hapo.

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW