BOT yaja na Mfumo Mpya wa kushughulikia malalamiko.

Na Yohani Gwangway.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo imetoa mafunzo kwa watoa huduma za kifedha kuhusu mfumo mpya ya kidijitali wa kushughulikia malalamiko ya wateja ambao unatarajiwa kuanza rasmi katikati ya mwezi Januari mwaka ujao 2025. Mafunzo haya yamefanyika katika Chuo cha BOT kilichopo eneo la Capri-Point jijini Mwanza.

Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili kwa watoa huduma za kifedha yaani Financial Service Providers(FSP’s), Mkurugenzi wa Benki Kuu tawi la Mwanza Gloria Mwaikambo amesema wameanzisha mfumo huo kutokana na changamoto ambazo wateja walikuwa wanazipata hapo awali.

“Kwahiyo kutokana  na changamoto mbalimbali wateja walikuwa wanazipata katika ushughulikiwaji wa malalamiko yao, BenkiKuu ikafikiria kuanzisha mfumo wa kielektroniki ambao utaenda kuondoa zile changamoto ambazo walikuwa wanakutana nazo” Alisema  Gloria Mwaikambo, Mkurugenzi wa BOT tawi la Mwanza.

Wakati wa mafunzo hayo, Mwaikambo alitaja changamoto za mfumo uliokuwepo hapo awali ambapo miongoni mwake ni wateja kuandika barua na kwenda nazo hadi Benki Kuu ili iweze kushughulikia malalamiko yake. Kutokana na hali hii wateja pamoja na taasisi za watoa huduma za kifedha (mabenki na nyinginezo) walikuwa wanapoteza muda kwa kusubiria changamoto zao zishughulikiwe.

Katika mfumo huu wa sasa wateja watapata faida kadhaa ikiwemo kupata huduma sehemu yoyote ile, huku wakiweza kujua hatua ambayo lalamiko lake limefikia. Faida nyingine ni kupata mrejesho kwa urahisi tofauti na zamani ambapo ilikuwa hadi ana kwa ana. Hapa nafafanua Mkurugenzi wa BOT tawi la Mwanza.

“Kwa hiyo mfumo huu utaondoa hizo changamoto, kwa maana ya kwamba wateja wataweza kupata huduma ya mfumo popote walipo, kitu cha pili wateja wanaweza kufuatilia hatua ambayo malalamiko yao yamefikia hukohuko walipo. Kitu kingine ambacho mfumo huu utakwenda kuboresha ni muda ambao malalamiko yao yanaenda kushughulikiwa. Kama tunavyofahamu ni kwamba teknolojia inakuja kurahisisha utendaji kazi, lakini vilevile kutakuwa na kumbukumbu ya malalamiko ya wateja kwenye mfumo”. Aliongeza Mwaikambo.

Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Tawi la Mwanza, Gloria Mwaikambo akizungumza na waandishi wa habari Disemba 18, 2024 kuhusu mafunzo hayo yanayotolewa na BOT jijini Mwanza kwa watoa huduma za kifedha.

Mfumo huo ambao unajulikana kama Mfumo wa kutatua na kushughulikia malalamiko ya kifedha wa BenkiKuu (Financial Complaints Resolution System-FCRS) kwa sasa upo katika hatua za majaribio huku BOT wakisema kuwa hata jina lililopo sasa ni la majaribio.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, taasisi za watoaji wa huduma za kifedha wamesema matarajio yao kuhusiana na mfumo huo mpya wa Benki Kuu ikiwa ni pamoja na kuokoa muda na kupunguza gharama. Meneja wa Mahusiano kwa wateja wa Bank of Africa Tanzania tawi la Mwanza, Baraka John Mwakaje anaamini mfumo huu utaboresha huduma zao.

“Nashukuru kwanza kwa huu mfumo ambao umeletwa na wazazi wetu, Benki Kuu na niseme tu sisi kama watoa huduma za kifedha utatusaidia sana. Moja utatusaidia katika urahisishaji wa kushughulikia  haya malalamiko kwa wateja, sisi pia tuna mfumo wetu wa malalamiko kwa wateja, kwahiyo mimi naamini mfumo wetu ukiungana na huu wa wazazi wetu BenkiKuu tutarahisisha kushughulika malalamiko ya wateja kwa haraka na kwa wepesi”. Alieleza Baraka Mwakaje kutoka Bank of Africa tawi la Mwanza.

Akiwakilisha baadhi ya watoa huduma waliohudhuria mafunzo hayo ya Benki Kuu, Baraka anaeleza kuwa katika njia za awali ambazo zilikuwa zikitumika kama kwenda ana kwa ana hadi Benki Kuu au kutumia barua zilikuwa zinachelewesha utoaji wa huduma.

“Changamoto mojawapo ni uchelewaji wa utatuzi wa malalamiko ya wateja, unajua kitu kinapokuwa katika hali ya kidijitali kunakuwa na uharaka zaidi, unajua kitu kikifanyika kidijitali kunakuwa na uharaka ukilinganisha nakutumia njia za manually (kawaida) kama makaratasi kama ilivyokuwa inafanyika awali. Tunaamini sasa hivi malalamiko ya wateja yatafanyiwa kazi kwa muda muafaka”. Baraka akielezea changamoto za awali akilinganisha na mfumo wa sasa.

Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kuendesha mafunzo hayo kwa watoa huduma za kifedha ambapo wameanza na mabenki kwa muda wa siku mbili na baadaye kutoa mafunzo hayo kwa taasisi ndogo za kifedha yaani Micro Finances hapa jijini Mwanza.

Madhumuni na malengo ya mfumo mpya wa Benki Kuu ni

  • Kuwapa wananchi majibu kwa wakati.
  • Unawafikia wananchi na watumiaji wa kifedhapopote walipo, ndani ya masaa 24, wakati wowote hivyo kuwa imara zaidi.
  • Unasaidia kutunza kumbukumbu za malalamiko kwa Benki Kuu.

Mfumo wa kidijitali wa BOT utakuwa na pande kuu 2 ambazo ni

  1. Upande wa wafanyakazi wa Benki Kuu- Internal users portal
  2. Upande wa watumiajiwa nje – Mabenki, micro finance, na wananchi wa kawaida

Katika mfumo huu mpya mteja wa Benki kuu atakuwa na uwezo wa kufahamu malalamiko yake yamefikia hatua gani (complaint status) kama ifuatavyo:

  1. Lalamiko limewasilishwa
  2. Lalamiko linafanyiwa kazi
  3. Lalamiko limetolewa uamuzi
  4. Lalamiko limefungwa na kutolewa mrejesho

Aina za walalamikaji katika mfumo mpya wa Benki Kuu ni

  1. Mlalamikaji binafsi
  2. Taasisi ya kifedha

Namna ya kutambua mlalamikaji katika mfumo mpya wa Benki Kuu

  1. Namba ya NIDA
  2. Usajili wa BRELA kwa taasisi au kampuni – namba ya usajili wa BRELA
  3. Namba ya simu
  4. Barua pepe

Lugha zitakazotumika katika mfumo mpya wa Benki Kuu ni

  1. Kiswahili
  2. Kiingereza

Mwandishi: Yohani Gwangway
Mhariri: Dominic Allen

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW