Tanzania yavuna USD Bilioni 4.4 Sekta ya Utalii

Na Dominic Allen

Mapato yatokanayo na shughuli za utalii Tanzania yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 3.9 mwaka 2024 hadi dola za Marekani bilioni 4.4 mwaka 2025, sawa na ongezeko la asilimia 12.82, ambapo ukuaji huo umeifanya sekta ya utalii kuwa chanzo cha pili kwa kuingiza fedha za kigeni nchini baada ya sekta ya madini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Mei 15, 2026, akieleza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa shughuli za utangazaji wa utalii, kuboreshwa kwa miundombinu pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika ukusanyaji wa mapato.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa idadi ya watalii nchini imefikia milioni 5.9 kwa mwaka 2025 kutoka watalii milioni 5.4 mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.7, ambapo watalii wa kimataifa wakiongezeka kutoka milioni 2.1 hadi milioni 2.3, huku watalii wa ndani wakiongezeka kutoka milioni 3.2 hadi milioni 3.6.

Kwa mujibu wa Shirikia la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika sekta hiyo duniani kwa kushika nafasi ya 11 kuwa na ongezeko la wageni wa kimataifa kwa asilimia 51 ikilinganishwa na mwaka 2019 kabla ya janga la UVIKO-19, huku ikishika nafasi ya sita katika ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati kwa ongezeko hilo la wageni wa kimataifa.

Picha: Habari Leo

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW