ACT Wazalendo: NAFRA ongezeni kasi ya kusambaza nafaka kuwapa ahueni kwa wananchi

Na Dominic Allen

Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme ametoa wito kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NAFRA) kuongeza juhudi za kuingiza chakula (nafaka) kwenye mzunguko ili kutoa unafuu wa bei za vyakula kwa wafanyabiashara na wateja.

Wito huo wa Waziri Kivuli, Mndeme umetolewa hapo jana mara baada ya kutembelea masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam, ambapo aliongozana na Naibu Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara, Julius Massabo.

Mndeme na Massabo walipata wasaa wa kutembelea soko la Mbagala, Buguruni na Mabibo na kuzungumza na wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa ili kujua changamoto mbalimbali wanazokutana zao katika biashara zao ikiwa ni pamoja na hali ya masoko hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Wafanyabiashara wamemueleza Waziri Kivuli, Mndeme kuwa hali ya miundombinu ya masoko hayo hairidhishi, huku kukiwa na changamoto ya upatikanaji wa wateja kutokana na mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.

Kwa upande wa wananchi, wamesema kuwa kwa kupanda kwa bei ya bidhaa ndani ya kipindi cha miezi mitatu imekuwa ni pigo kwao, wakitolea mfano wa bei ya unga wa ugali ambayo imepanda kutoka Tsh. 1,000 kwa kilo hadi Tsh. 1,400; mchele kutoka Tsh. 1,400 kwa kilo hadi Tsh. 3,000 huku mafuta kupikia yakipanda kutoka Tsh. 4,500 kwa lita hadi Tsh. 5,000.

Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme pamoja na Naibu wake, Julius Massabo wakizungumza na wafanyabiashara katika moja ya masoko waliyotembelea Machi, 14, 2025. Picha na ACT Wazalendo.

Waziri Kivuli, Mndeme ameeleza kuwa taarifa za uchumi zinaonesha kuwa mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji visivyokuwa na kilevi umeongezeka kutoka asilimia 4.6 mwezi Disemba 2024 hadi asilimia 5.3 mwezi Januari 2025, jambo limewasukuma kufanya ziara hiyo kwenye masoko.

Mndeme pia ameonesha kutoridhishwa na hali ya usafi kwenye masoko hayo na kuzitaka Halmashauri za Temeke, Ilala na Kinondoni kushirikiana na uongozi wa masoko na kuwa na programu maalum ya usafi na kuboresha mazingira ili shughuli zifanyike kwa usalama zaidi.

Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme akikagua hali ya usafi katika soko. Picha na ACT Wazalendo.

Mwandishi: Dominic Allen

Mhariri: Yohani Gwangway

Hot this week

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW