Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amethibitisha kutokea kwa ajali ya barabarani iliyohusisha lori lililokuwa limebeba miti aina ya mirunda na basi la abiria, ambapo magari hayo yaligongana na kuteketea kwa moto.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkambarani, Halmashauri ya Morogoro, kwenye Barabara Kuu ya Morogoro–Dar es Salaam.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, ACP Kantimbo amesema watu 30 wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku idadi kamili ya waliopoteza maisha ambapo wanne wakihofiwa kutokana na baadhi ya miili kuteketea kwa moto.
Kuhusu chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Kantimbo amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori, anayedaiwa kujaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari za kutosha.
Picha: Millard Ayo


