Baadhi ya wakazi wa tarafa za Loliondo na wanadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi

Baadhi ya wakazi wa tarafa za Loliondo na wanadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kujitokeza na kuomba kuundwa kwa tume jumuishi ya kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya nzima ya Ngorongoro badala ya kuundwa kwa tume katika baadhi ya tarafa.

Wananchi hao walijitokeza na kusema kuwa katika tume mbili zilizoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hazijagusa wilaya nzima ya Ngorongoro hasa tarafa za Loliondo na Sale, ambapo zimeegamia upande mmoja wa tarafa ya Ngorongoro, licha ya kuwepo kwa changamoto za migogoro ya ardhi katika tarafa za Loliondo na Sale ambapo walimuomba Rais Samia kuunda tume nyingine itakayoshughulikia changamoto katika tarafa hizo.

Nao Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema kuwa licha ya wananchi hayo kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kuna baadhi yao wameandikiwa barua ya wito katika kikao cha Kamati ya Usalama ya Wilaya.

“Kinachotushangaza ni kwamba wananchi wa Loliondo ambao wametoa maoni yao kama Watanzania wengine wameitwa polisi, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Wilaya ya Ngorongoro ameitwa polisi kwa kutoa maoni yake, akawekwa ndani kwa muda mchache”. Amesema Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu kitaifa wa THRDC.

Hata hivyo THRDC imelaani vitendo hivyo vinavyokiuka haki za binadamu, kwani wananchi hao wametekeleza haki yao ya kikatiba, lakini pia ni imetafsiri vitendo hivyo kuwa ni vitisho dhidi ya wananchi na wanaharakati ambao wamekuwa mstari wa mbele kuzisemea jamii.

“Tume hizi zinakwenda kugusa maisha yao kama wananchi wa wilaya ya Ngorongoro, hivyo ilikuwa ni haki kwa wananchi wa Ngorongoro kwanza kupongeza uwepo wa tume hizi kama walivyofanya, lakini kwenda mbali zaidi kutoa maoni kuhusu muundo wa tume hizi”. Amesema Wakili Olengurumwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao wamesema kuwa badala ya tume hizo kujaa watumishi wa serikali, wamemuomba Rais Samia uwepo ushiriki wa wananchi kwa asilimia kubwa katika uundaji wa tume hizo, Asasi za Kiraia, viongozi wa mila na viongozi wa kidini.

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kukamatwa kwa wananchi hao wa tarafa za Loliondo na Sale, Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Kanali Wilson Sakulo amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa hakuna aliyekamatwa.

Chanzo: Jambo TV

Hot this week

CHADEMA kutoa msimamo wake kuhusu maridhiano

By Veronica Mlyatu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa...

Mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni

By Dorlingson Edward Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), leo...

Popular Articles

Safari ya Mashimba katika kutetea jamii ya Wahadzabe

Nchini Tanzania  kuna jumla ya makabila zaidi ya 120...

Polisi waendelea kuwashikilia viongozi wa CHADEMA

Ni siku ya kwanza tangu kukamatwa kwa viongozi wa...

Siku ya Vijana Duniani.

Kwa sasa ni kijana wa miaka 25 ambaye amejiajiri...

BWAWA LA ARBA’AT  LASABABISHA MAAFA NCHINI SUDAN

Watu 30 mashariki mwa Sudan na na wengine 60...

Sand Mining in Tanzania: Trails of Destruction in Lake Victoria and its Environs

By Dominic Allen On November 14th, 2021 in the Geita...

 Utekaji: Fumbo linalotushinda?

Na Yohani Gwangway Taifa la Tanzania kwa miaka mingi limekuwa...

Abduction: Is it a riddle we can’t solve?

By Yohani Gwangway For many years Tanzania has been an...

Mustakabali wa Hewa Safi kwa kila kiumbe

Na Dominic Allen Msingi wa maisha ya viumbe hai yaani...
LAND DWELLERS FACT CHECK HUB VERIFY FACTS STOP MISINFORMATION Trusted Fact-Checking in Tanzania Beyond What You Know VERIFY NOW

Related Articles

Popular Categories

DWELLERS CHECK-HUB Verify Facts. Stop Misinformation Trusted Fact-Checking in Tanzania • Beyond What You Know VERIFY NOW